Upatanisho
Upatanishi ni mchakato Mbadala wa Utatuzi wa Migogoro ambapo mtu wa tatu huru, mpatanishi, huwasaidia watu katika mgogoro kutambua masuala yenye mgogoro, kubuni machaguo, kufikiria njia mbadala na kujaribu kufikia makubaliano.
Mpatanishi anaweza kuwa na utaalamu wa suala lenye mgogoro na kwa ujumla atatoa ushauri kuhusu masuala na machaguo ya utatuzi. Hata hivyo, mpatanishi hatatoa hukumu au uamuzi kuhusu mgogoro huo.
Upatanisho unaweza kuwa wa hiari, kuamriwa na mahakama au kuhitajika kama sehemu ya mkataba. Mara nyingi huwa ni sehemu ya mchakato wa mahakama au wakala wa serikali.
Kuhusu mchakato wa upatanishi
Wajibu wa wapatanishi ni sawa na wa wasuluhishi isipokuwa mpatanishi anaweza pia:
- Kuwa na ujuzi wa kitaalamu na kukupa taarifa za kisheria
- Kupendekeza au kukupa wewe na washiriki wengineushauri wa kitaalamu kuhusu machaguo yanayowezekana ya kutatua masuala katika mgogoro wako.
- Kukuhimiza kikamilifu na washiriki wengine kufikia makubaliano.
Mpatanishi hatafanya yafuatayo:
- Kuwa upande fulani au kufanya uamuzi
- Kukuambia uamuzi wa kufanya, ingawa wanaweza kutoa mapendekezo
- Kuamua ni nani aliye sahihi au asiye sahihi
- Kutoa unasihi.
Upatanishi kawaida hufanyika ana kwa ana, ili muweze kuzungumza moja kwa moja. Hata hivyo, unaweza pia kuwa na vikao na msuluhishi peke yenu.
Wakati mwingine mpatanishi anaweza kufanya kama 'mjumbe' kwa kuzungumza na wewe na washiriki wengine peke yao na kuwasilisha mawazo au mapendekezo kati yenu. Inawezekana pia kufanya vikao vya upatanishi kwa njia ya simu katika hali fulani.
Upatanishi unafaa lini?
Upatanishi unaweza kufaa ikiwa:
- Unataka kufikia makubaliano kuhusu baadhi ya masuala ya kitaalamu na kisheria
- Unataka usaidizi katika mchakato
- Unataka kufanya uamuzi na washiriki wengine wanaohusika
- Unataka ushauri kuhusu ukweli katika mgogoro wako.
- Upatanishi unaweza pia kufaa ikiwa umejaribu usuluhishi na bado huwezi kufikia makubaliano na washiriki wengine.
Wanasheria au wataalamu wana jukumu gani?
Wanasheria wa washiriki kwa kawaida wanaweza kuwapo wakati wa upatanishi. Katika baadhi ya matukio, wataalamu wanaweza pia kuwapo. Baadhi ya michakato ya upatanishi haihitaji wanasheria kushiriki. Ikiwa ungependa kuwa na wakili wako kushiriki katika mchakato wa upatanishi au kuwa na wataalamu, unapaswa kujadili hili na msuluhishi kabla ya mchakato kuanza.