Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

TAASISI YA USULUHISHI WA MALALAMIKO NA TAARIFA ZA KODI

"Haki na Usawa"

Dira na Dhamira

Kauli Yetu Inayotuongoza

Kama Ofisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi, tunajitahidi kuoanisha shughuli zetu, mikakati, sera, muundo na utendaji wetu ili kuhakikisha kwamba tunakuwa taasisi ambayo walipa kodi wanaweza kuitegemea na kuiamini. Sisi ni nani, tunathamini nini, tunafanyaje, na tunakokwenda ndio msingi wa Dira, Dhamira na Maadili yetu.

Dira

Kuwa kitovu cha ubora, kutumainiwa, kuwa na uaminifu na kutegemewa katika kushughulikia malalamiko ya walipa kodi

Dhamira

Kuwa taasisi yenye malengo, ufanisi, uhuru, uadilifu, njia za haki na usawa kwa malalamiko ya walipa kodi