Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

TAASISI YA USULUHISHI WA MALALAMIKO NA TAARIFA ZA KODI

"Haki na Usawa"

Types of complaints

1. Malalamiko ya Huduma

Ni malalamiko yanayotokea pale mhusika katika kituo cha utoaji wa huduma anaposhindwa kutekeleza sehemu yake ya kanuni na masharti ambayo yanaunda uhusiano uliopo kati yao.

2. Malalamiko ya Kiutaratibu

Haya ni malalamiko ambayo yanajitokeza pale ambapo mlipakodi au Kamishna Mkuu, TRA au wafanyakazi wanapokiuka taratibu wakati wa kutekeleza majukumu yaliyowekwa kisheria.

3. Malalamiko ya Utawala

Haya ni malalamiko yanayotokea pale ambapo mhusika katika uamuzi wa kiutawala anapotumia mamlaka ambayo hayajaidhinishwa kisheria kukiuka haki ambayo imewekwa kisheria.